Dec 2, 2016

WATAKAOKUTWA na VVU Waanze ARVs Mara Moja-Waziri

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeagiza wale wote ambao wanakutwa na maambukizi ya VVU, waanze kupata huduma ya dawa za ARVs mara moja.

Kauli hiyo imetolewa mapema leo na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo huadhimishwa ifikapo Desemba Mosi  ya kila mwaka.

Mwalimu alisema utaratibu huo umekuja ili kuwafanya wenye maambukizi waweze kuishi maisha marefu na yaliyo na afya bora.

"Maelekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) yanazitaka nchi zetu kuwaanzishia dawa mara moja watu wote watakaopima na kugundulika wana VVU, yaani “Test and Treat”," alisema Mwalimu.Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR