• Breaking News

  Feb 7, 2017

  Kauli Walizotoa Viongozi Kumi Kuhusu Vita Dhidi ya Madawa ya Kulevya

  “Katika vita hii ya madawa ya kulevya, hakuna cha mtu aliye maarufu, hakuna mwanasiasa, hakuna askari, hakuna waziri au mtoto wa fulani ambaye akijihusishwa aachwe. Hata kama angekuwa mke wangu Janeth, akijihusisha shika.”

  Paul Makonda (Mkuu wa Mkoa, Dar es salaam

  “Haya mapambano si ya mtu mmoja na kelele nyingine mnazozisikia zinatupa hamasa tuendelee kufanya kazi. Tunachotafuta sisi ni majibu, tukifika mbinguni tumweleze Mungu kwamba dhamana uliyotupa tuliitendea haki.”

  Nape Nnauye (Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo)

  “Ni muhimu kulinda haki ya mtuhumiwa. Jambo lenye mjadala ni busara inayotumika kushughulika na wahusika ili kusaidia vyombo vyengine kuwataja wanaosambaza. Tusiwahukumu kwa tuhuma maana wasanii kujenga ‘brand’ (jina) ni kazi kubwa ila kubomoa jina ni sekunde tu. Ni vizuri tukaangalia, tufanye katika namna ya kumlinda mtuhumiwa ili hata kama hahusiki jina lake lisiporomoke.”

  Kamishna Simon Siro (Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es salaam)

  “Hata hao wanaosema wana ‘brand’ kubwa wamejitahidi kutoa ushirikiano na wako waliokamatwa na vielelezo, wengine wamekiri kutumia na wametusaidia sana kwenda kuwakamata wanaouza. Nimejitahidi mwenyewe kuwahoji mmoja mmoja, niliona kuwapa wapelelezi wawahoji wanaweza wasitende haki…mimi ni kachero mzoefu.”

  Esther Bulaya (Mbunge wa Bunda Mjini)

  “Namshauri mdogo wangu Makonda, hao anaowakamata na kuwaweka ndani ni watu wadogo sana, badala yake awakamate mapapa ambao ndio wanaoingiza dawa hizo. Makonda akamuone mama Leila kule gerezani, akamueleze dawa zinavyoingizwa nhini kwa sababu hao anaowakamata ni wale wanaotakiwa kuwa Mwananyamala au Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.”

  Goodluck Mlingwa (Mbunge wa Ulanga)

  “Wafanyabiashara wa madawa ya kulevya hamna asiye wajua, tuna wajua. Humu ndani wapo, nje ya Bunge wapo.”

  Joseph Msukuma (Mbunge wa Geita Vijijini)

  “Kwa nini vyombo vya dola visimchunguze Makonda maana anasafiri sana Ulaya na Dubai, hivi anasafiri kwa mshahara upi alionao? Kama Rais Magufuli amesema kama mkewe Mama Janeth anahusika na dawa za kulevya akamatwe, kwanini Makonda naye asihojiwe kwa sababu amewapangishia watu nyumba wakati wanajihusisha na dawa za kulevya?”

  Halima Mdee (Mbunge wa Kawe)

  “Hapa tusitafute ‘headline’ kwenye vyombo vya habari, lazima tuwe na ‘political will’ (utayari wa pamoja wa kisiasa), tuache usanii. Kama mheshimiwa Rais hawajakwambia, basi ujue kwenye kampeni zako ulichangiwa na hao wauza dawa za kulevya. Nchini sasa tuna njaa, kwahiyo mnachotaka kufanya ni kubadili akili za Watanzania kwa hizi mbwembwe zenu. Mnasema Wema Sepetu anahusika na dawa za kulevya wakati alizunguka na Makamu wa Rais kwenye kampeni  kwa miezi yote mitatu.”

  Hussein Bashe (Mbunge wa Nzega Mjini)

  “Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete alisema anayo orodha ya wafanya biashara wa dawa za kulevya. Kwakuwa alisema anayo, namuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amfuate Kikwete pale kijijini kwake Msoga ampe hiyo orodha ili waungane na kasi ya Makonda ya kupambana na dawa hizo. ”

  Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Mjini)

  “Ukiona kifaranga kipo juu ya chungu ujue chini kuna mama yake, leo Rais ametamka kuwa vita ile sio ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam peke yake bali ni vita ya wote. Vita ya wote kuendeshwa na Mkuu wa Mkoa mmoja ni jambo la kushangaza kidogo, lakini halina ubaya kwani lazima awepo wa kubutua kombolela.”

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku